#Business

WAKENYA KUTOA MAONI KUHUSU MSWAADA WA KIFEDHA 2026/27

Umma unatarajiwa kuwasilisha maoni yao kuhusu hatua za ushuru na vipaumbele vya bajeti baada ya Hazina ya Kitaifa kutoa ilani kwa umma kutaka maoni yao kabla ya bajeti ya mwaka wa kifedha wa 2026/27 kuwasilishwa bungeni.

Mashauriano hayo yanakuja wakati muhimu wakati serikali inazingatia marekebisho makubwa ya kodi, ikiwa ni pamoja na mapitio yanayoweza kujitokeza ya Pay-As-You-Earn (PAYE), yanayotarajiwa kuandikwa katika Mswada ujao wa Fedha wa 2026.

Notisi hiyo, ambayo imetolewa na Waziri wa Hazina ya kitaifa John Mbadi, inaashiria awamu ya mwisho ya ushiriki wa umma kabla ya bajeti kuwasilishwa Bungeni mwezi Juni. Bajeti hiyo inaangazia sehemu muhimu ambapo wananchi, wafanyabiashara na washikadau wa sekta mbali mbali wanaweza kupendekeza mabadiliko, ikiwa ni pamoja na vipaumbele vya kodi, sera ya uchumi na matumizi.

Kulingana na waraka huo, Hazina inatafuta mapendekezo ya kusawazisha uzalishaji wa mapato na kupunguza mzigo kwa mwananchi na biashara mbali mbali, huku kukiwa na wasiwasi juu ya gharama ya maisha.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

WAKENYA KUTOA MAONI KUHUSU MSWAADA WA KIFEDHA 2026/27

UPINZANI WAELEKEA KWALE 

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *