UPINZANI WAELEKEA KWALE
Viongozi wa muungano wa upinzani nchini wameimarisha juhudi za kusaka uungwaji mkono kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, hii leo wakielekea katika kaunti ya Kwale siku moja baada ya kukamilisha ziara ya siku 2 katika kaunti ya Kitui.
Wakiongozwa na kinara wa DCP Rigathi Gachagua, viongozi hao wameratibiwa kutangamana na wananchi katika maeneo ya Samburu na Kinango kabla kukamilishia ziara yao mjini Kwale.
Katika ziara zao za awali, viongozi hao wamekuwa wakiikosoa serikali kutokana na changamoto za kiuchumi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































