#Local News

ASIGE AANGAZIA KUTENGWA KWA WATU WENYE ULEMAVU

Seneta mteule Crystal Asige ameibua wasiwasi bungeni kuhusu kutengwa kwa watu wenye ulemavu katika mifumo ya usajili nchini akisema hali hiyo inawanyima haki zao za msingi

Asige amesisitiza kuwa mamilioni ya watu bado hawana vitambulisho vya kitaifa vyeti vya ulemavu pamoja na usajili wa wapiga kura jambo linalowazuia kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia

Aidha amesema ni muhimu serikali kuchukua hatua za haraka kuhakikisha usawa uwajibikaji na ujumuishaji ili kuwapa watu wenye ulemavu fursa sawa katika masuala ya utawala na maendeleo nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

ASIGE AANGAZIA KUTENGWA KWA WATU WENYE ULEMAVU

RUTO AWAKOSOA WANAOCHOCHEA UMMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *