#Local News

IEBC YASISITIZA MWISHO WA USAJILI WA WAPIGA KURA NI APRILI 28

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imesisitiza kuwa zoezi la usajili wa wapiga kura halitaongezewa muda na litakamilika Aprili ishirini na nane mwaka elfu mbili ishirini na sita.

Akizungumza katika eneo la Iten Kaunti ya Elgeyo Marakwet,  Mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon ameonya dhidi ya kuingiza siasa katika mchakato huo akisisitiza kuwa unapaswa kubaki huru na wa haki kwa wote.

Amehakikisha kuwa tume imejizatiti kuwafikia wananchi wote wanaostahili kujiandikisha huku akiwahimiza kujitokeza kwa wingi kabla ya muda uliopangwa kukamilika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

IEBC YASISITIZA MWISHO WA USAJILI WA WAPIGA KURA NI APRILI 28

NDEGE YAPATA AJALI MANDERA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *