#Local News

NDEGE YAPATA AJALI MANDERA

Ndege aina ya Embraer inayomilikiwa na kampuni ya EBB Air imehusika katika tukio la kutoka nje ya njia ya kutua katika uwanja wa ndege wa Mandera siku ya Ijumaa Aprili ishirini na nne,

Ndege hiyo iliyokuwa imetoka Nairobi kuelekea Mandera iliteleza na kusimama katika vichaka vilivyo karibu na uwanja huo baada ya kushindwa kusimama ndani ya njia ya kutua hata hivyo abiria na wahudumu wote wamethibitishwa kuwa salama,

Timu za dharura zilifika haraka eneo la tukio na zinaendelea kushughulikia hali hiyo huku mamlaka husika zikianzisha uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo kabla ya shughuli za kawaida za uwanja huo kurejea kawaida.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *