#Local News

UPINZANI WATAKA FIDIA KAMILI KWA WAATHIRIWA WA MAANDAMANO

Viongozi wa upinzani wameitaka serikali kuangazia upya suala la fidia kwa waathiriwa wa maandamano wakisisitiza kuwa wanapaswa kulipwa kikamilifu kulingana na hasara walizopata.

Wakizungumza katika mikutano ya kisiasa kaunti ya Kwale viongozi hao pia wameikosoa serikali wakidai imeshindwa kushughulikia ipasavyo changamoto ya gharama ya juu ya maisha inayowaathiri wananchi wengi.

Aidha wamehimiza serikali kuchukua hatua za haraka kuboresha hali ya uchumi na kuhakikisha haki inatendeka kwa waathiriwa huku wakiahidi kuendelea kushinikiza mabadiliko kupitia majukwaa ya kisiasa.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

UPINZANI WATAKA FIDIA KAMILI KWA WAATHIRIWA WA MAANDAMANO

NDEGE YAPATA AJALI MANDERA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *