#Local News

ZIARA YA RUTO MURANG’A YACHOCHEA MIRADI YA MAENDELEO

Ziara ya Rais William Ruto katika Kaunti ya Murang’a imesifiwa na viongozi mbalimbali kwa kuchochea utekelezaji wa miradi muhimu ya maendeleo katika eneo hilo.

Viongozi hao wamesema ziara hiyo imeleta msukumo mpya katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu na huduma za kijamii wakihusisha hatua hiyo na dhamira ya serikali ya kuharakisha maendeleo mashinani.

Aidha wameeleza kuwa miradi inayoendelea na ile inayotarajiwa itachangia kuboresha maisha ya wananchi huku wakihimiza ushirikiano kati ya serikali na jamii ili kuhakikisha mafanikio ya muda mrefu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *