#Sports #Volleyball

KCB YAJIVUNIA NAFASI YA PILI AFRIKA

Nahodha wa timu ya voliboli ya KCB Mercy Moim pamoja na mlezi wa timu hiyo Judith Sidi Odhiambo wameeleza fahari na azma baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye mashindano ya klabu bingwa Afrika yaliyofanyika Cairo Misri.

Moim amewapongeza wachezaji wenzake kwa uthabiti wao katika mashindano hayo magumu licha ya kupoteza fainali kwa seti tatu kwa moja dhidi ya Al Ahly ya Misri akisema uzoefu huo utawapa motisha ya kufanya vizuri zaidi siku zijazo.

Kwa upande wake Odhiambo amesema medali ya fedha ni hatua muhimu kwa maendeleo ya klabu hiyo akisisitiza kuwa timu itaendelea kujipanga upya ili kufikia ndoto ya kutwaa ubingwa wa Afrika katika mashindano yajayo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *