MARESCA AIBUKA CHAGUO KUU KURITHI GUARDIOLA MAN CITY
Kocha Raia wa Italia Enzo Maresca anaendelea kutajwa kama chaguo kuu la kuinoa Manchester City endapo Pep Guardiola ataondoka katika nafasi hiyo.
Viongozi wa klabu hiyo wanaamini Maresca ndiye anayefaa kuendeleza falsafa ya timu hiyo huku wakisubiri uamuzi wa Guardiola kuhusu mustakabali wake.
Licha ya vilabu kadhaa vya Italia kuonyesha nia ya kumtaka hakuna makubaliano yaliyofikiwa bado huku Manchester City ikiendelea kuweka mikakati ya muda mrefu kuhusu nafasi ya ukocha.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































