ASKARI POLISI ANATAFUTA HAKI KATIKA MALI YA MAMILIONI YA BABUYE
Askari polisi mwenye umri wa miaka 55 amewasilisha kesi katika Mahakama Kuu mjini Eldoret akitaka umiliki wa mali ya babu yake aliyefariki miaka minane iliyopita.
Stanley Kibet Kogo, ambaye anaishi katika kituo cha polisi cha Yamumbi katika kaunti ndogo ya Kesses amewashtaki wajomba zake, Emmanuel Kiptoo Lamai na Benjamin Kiptoo Lamai kwa kumbagua katika ugawaji wa mali ya marehemu Alfred Kaplamai Bor.
Imetayarishwa na Janice Marete
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































