#Football #Sports

ADUDA AONYA MVUTANO FKF WATISHIA AFCON 2027

Aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) Lodvick Aduda ameonya kuwa Kenya inaweza kuhatarisha nafasi yake ya kuandaa michuano ya Mataifa ya Afrika 2027 kutokana na mvutano unaoendelea ndani ya shirikisho hilo.

Mvutano huo unamkabili Rais wa FKF Hussein Mohammed na naibu wake McDonald Mariga kufuatia madai ya kashfa ya bima ya mashindano ya CHAN 2024.

Aduda ametoa wito wa utulivu na maelewano ndani ya uongozi wa FKF akionya kuwa mzozo huo unaweza kudhoofisha maandalizi na kuharibu taswira ya Kenya kimataifa, jambo ambalo linaweza kuathiri juhudi za kuandaa kwa mafanikio mashindano ya AFCON 2027.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *