BEI YA TANI YA MIWA YASHUKA
Bodi ya Sukari ya nchini imetangaza marekebisho ya kushuka kwa bei ya miwa, na kupunguza kiwango hicho kutoka Ksh5,750 hadi Ksh5,500 kwa tani.
Katika notisiambayo imetolewa , kufuatia mikutano ya Kamati ya Muda ya Kupanga Bei ya Miwa iliyofanyika Aprili 17 na Aprili 24, mwaka huu bodi imethibitisha kwamba bei mpya ya chini ya Ksh5,500 kwa tani itaanza kutumika mara moja.
Agizo hilo ambalo limetiwa saini na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Jude Chesire, linawaagiza wasagaji wote kuzingatia kiwango kilichorekebishwa na kuhakikisha malipo ya wakulima kwa wakati.
Vile vile Uamuzi huo umebadilisha bei ya juu ya hapo awali ya Ksh5,750 kwa tani, na hivyo kuzua wasiwasi juu ya kutofautiana kwa sera na athari za kifedha kwa wakulima wa miwa ambao walitarajia kuboreshwa kwa mapato huku kukiwa na kupanda kwa gharama za uzalishaji.Hata hivyo, bodi hiyo inahoji kuwa bei mpya iliyowekwa bado iko juu ikilinganishwa na nchi jirani za kanda ya afrika mashariki.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































