SERIKALI YATAKA USHIRIKIANO NA WAENDESHA BODABODA KUIMARISHA USALAMA
Katibu Mkuu wa Usalama wa Ndani Raymond Omollo amewahimiza waendesha bodaboda kote nchini kushirikiana na vyombo vya usalama katika juhudi za kukabiliana na ongezeko la ukosefu wa usalama.
Akizungumza Kaunti ya Homabay, Omollo amesema serikali inapanga kutumia waendesha bodaboda kama watoa taarifa muhimu ili kusaidia kubaini na kuripoti shughuli za uhalifu kwa wakati akionya kuwa wachache wanaojihusisha na uhalifu wasiharibu taswira ya sekta nzima,
Aidha amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa jamii kwa ujumla katika masuala ya usalama.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































