HOFU YATANDA TSEIKURU BAADA YA UVAMIZI
Maafisa wa usalama wameanzisha msako dhidi ya washukiwa wa uvamizi uliotekelezwa katika kijiji cha Kwa Kamari kaunti ya Kitui Jumamosi, na kusababisha vifo vya watu 7, serikali ikisema uvamizi huo ni sehemu ya mashambulizi ya kulipiza kisasi kati ya jamii za wafugaji na wakulima eneo la Tseikuru.
Wakazi ambao wameingiwa na hofu, wamesema wavamizi wanaoshukiwa kutoka jamii ya wafugaji, waliwavamia wafanyabiashara katika soko la Kwa Kamari kwa panga kabla ya kuteketeza biashara.
Naibu Inspekta mkuu wa polisi Eliud Lagat, amezuru eneo hilo na kutangaza msako dhidi ya wavamizi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































