MAHAKAMA KUANZA VIKAO VYA KESI YA GACHAGUA
Vikao vya siku 3 vya kusikiliza kesi ambapo aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua anapinga kutimuliwa kwake kutoka afisini vinaanza hii leo mbele ya jopo la majaji 3, Gachagua akisema ana imani kwamba atapata haki.
Wakati uo huo, viongozi wa muungano wa upinzani wamelitaka jopo hilo la mahakama kuu kuangazia kwa makini sababu za kutimuliwa kwake, wakisema mchakato wa kumtimua ulikumbwa na dosari kutoka mwanzo.
Wameshikilia kuwa mchakato huo ulichochewa kisiasa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































