#Local News

UTABIRI WAONYA MVUA KUBWA KUENDELEA

Wakenya wametakiwa kuchukua tahadhari kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika mengi ya maeneo ya nchi, mafuriko ya ghafla na matatizo ya kuona vizuri barabarani yakihofiwa.

Kwenye ripoti yake, idara ya utabiri wa hali ya anga imebashiri kuwa mvua itaendelea kunyesha hadi tarehe 4 mwezi ujao, katika maeneo kadhaa ikiwemo nyanda za juu za maeneo ya mashariki, bonde la ufa, Homa Bay, Bungoma, Kisii, Kakamega, West Pokot, Nakuru, Nairobi, pwani na kaskazini mashariki.

Imeonya kuwa mito katika maeneo ambayo hayapokei mvua kubwa moja kwa moja pia inaweza kufuriki, na kuwataka madereva kuwa makini kutokana na matatizo ya kuona barabarani.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

UTABIRI WAONYA MVUA KUBWA KUENDELEA

MASOMO JSS NJIA PANDA MUHULA HUU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *