#Football #Sports

CARRICK HANA WASIWASI NA SAFU YA ULINZI

Kocha wa Manchester United Michael Carrick amesema hana wasiwasi wowote kuhusu eneo la beki wa kati kuelekea dirisha la usajili wa majira ya kiangazi, akisisitiza kuwa kwa sasa si kipaumbele kikubwa kwa timu.

Carrick pia amefichua kuwa alikutana na mmiliki mwenza wa klabu Sir Jim Ratcliffe katika uwanja wa mazoezi wa Carrington ambapo walifanya mazungumzo ya kirafiki, akieleza kuwa ni jambo zuri kuona uongozi ukionyesha msaada.

Ameongeza kuwa mshikamano ndani ya klabu ni muhimu sana na kwamba uhusiano mzuri kati ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji ndio msingi wa mafanikio ya muda mrefu.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *