WALIMU VIHIGA WATOA NOTISI YA MGOMO KUHUSU SHA
Walimu katika Kaunti ya Vihiga wametoa notisi ya siku 14 kwa Wizara ya Afya pamoja na Tume ya Kuwaajiri Walimu (TSC) kutatua changamoto zinazohusiana na bima ya afya ya SHA au waanze mgomo.
Kupitia chama cha walimu KUPPET walimu hao wamesema wamekuwa wakihangaika mara kwa mara wanapotafuta huduma za matibabu.
Wamesisitiza kuwa iwapo matatizo hayo hayatashughulikiwa ndani ya muda uliotolewa watachukua hatua ya kusitisha kazi wakitaka maboresho ya haraka katika mfumo wa SHA ili kuhakikisha wanapata huduma bora za afya.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































