GACHAGUA APIGA ABAUTANI KWENYE KESI YA KUTIMULIWA
Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua sasa amefutilia mbali ombi lake la kutaka arejeshwe afisini jinsi alivyokuwa amewasilisha kesi inayoendelea kwa sasa katika mahakama ya Milimani, na badala yake anataka kupewa fidia.
Wakati wa vikao vinavyosikilizwa na majaji Anthony Mrima, Freda Mugambi na Erick Ogolla, mawakili wa Gachagua wameiarifu mahakama kwamba kesi hiyo iliyofanyiwa marekebisho sasa haitaki kurejeshwa kwake afisini.
Badala yake, anataka mahakama iamuru fidia pamoja na amri kwamba kutimuliwa kwake kulikiuka sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































