#Local News

UDA MATATANI KWA ‘KUKWEPA’ KULIPA KODI

Tume ya kutetea haki za kibinadamu, KHCR imetishia kukishtaki mahakamani chama tawala cha UDA kutokana na madai ya kukwepa kulipa kodi na madai ya kuhusika katika matumizi mengine mabaya ya fedha za umma.

Ikinukuu ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali, KHCR imesema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari kwamba ripoti hiyo inafichua uvunjaji wa sheria na kushindwa kutimiza majukumu ya kodi, ikiapa kuchukua hatua dhidi ya UDA na maafisa wake.

Inaituhumu UDA kwa kulipa zaidi ya shilingi milioni 120 kama mishahara ila ikashindwa kuwasilisha makato ya Pay as you Earn, PAYE.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *