#Local News

MASOMO JSS NJIA PANDA MUHULA HUU

Muhula wa pili katika shule za msingi na upili umeingia siku ya pili huku wazazi na wanafunzi wa sekondari msingi, JSS wakiachwa kwenye njia panda kutokana na mgomo wa walimu wa shule hizo, ambao wametishia kuendelea na mgomo hadi malalamishi yao yatakapotatuliwa.

Miongoni mwa matakwa ya walimu hao waliofanya maandamano hapo jana, ni walimu 44,000 kupewa ajira ya kudumu, mgomo wao ukiungwa mkono na walimu wengine wanaolalamikia bima ya afya SHA licha ya hakikisho la wizara ya afya kwamba changamoto za bima hiyo zitatatuliwa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *