#Local News

ORENGO AJITANGAZA KINARA WA ODM

Utata wa uongozi umeendelea kujitokeza ndani ya chama cha ODM, gavana wa Siaya James Orengo akijitangaza kuwa kaimu kinara wa chama hicho, wadhifa unaoshikiliwa na seneta wa kaunti hiyo Oburu Oginga.

Wakizungumza jijini Kisumu wakati wa mkutano wa Linda Mwananchi ulioongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna, viongozi wa mrengo huo wameikosoa serikali kwa kukosa kutekeleza ajenda 10 zilizotiwa saini na Rais William Ruto na kinara mwanzilishi wa ODM marehemu Raila Odinga.

Wameshikilia kwamba Oburu anashikilia wadhifa huo kinyume na sheria.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *