#Football #Sports

SYPHAS OTIENO ANG’ARA AKIWA AMERUDI KUTOKA MAJERAHA

Mshambuliaji wa Migori Youth Syphas Otieno ameonyesha furaha yake baada ya kurejea uwanjani kufuatia majeraha na kuchangia pakubwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Nzoia Sugar FC katika mechi ya National Super League mwishoni mwa wiki.

Otieno ambaye alikuwa nje kwa wiki tatu alicheza dakika 10 za mwisho lakini alifanya athari ya haraka kwa kufunga bao lililokamilisha ushindi huo mkubwa wa Migori Youth.

Bao hilo limemrejesha kileleni mwa orodha ya wafungaji bora akiwa na mabao 18, akilingana na Collins Mwangi katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Golden Boot ya ligi hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *