#Football #Sports

BB BREAD YABOMOA GOR, AFC LEOPARDS

Timu ya BB Bread kutoka mtaani Kayole imesimamisha safari ya Gor Mahia kuelekea fainali za FKF Cup walikofika msimu jana na kupoteza kwenye fainali dhidi ya Nairobi United.

Baada ya kuwabandua AFC Leopards katika Raundi ya 64, BB Bread iliibua mshtuko mwingine wa kuwabandua miamba wa soka, mara hii wakiicharaza Gor Mahia bao 1-0 katika Raundi ya 32, na kujikatia tiketi ya Raundi ya 16.

Bao la pekee la mchezo katika dakika ya 84 kupitia kwa nguvu mpya Dennis Muthini lilitosha kuidhalilisha Gor Mahia, na kuwapa ushindi muhimu vijana hao wanaoshiriki ligi ya FKF tawi la Nairobi Mashariki.

Bingwa wa FKF Cup atashiriki dimba la mashirikisho barani Afrika msimu ujao.

Timu nyingine zilizofuzu raundi ya 16 ni Tusker FC, Shabana FC, Kenya Police, Ulinzi Stars, bingwa mtetezi Nairobi United, Kariobangi Sharks, Murang’a Seal, Kakamega Homeboyz, Bandari na Posta Rangers- zote za ligi kuu.

Nyingine ni 3k FC inayoshiriki ligi ya National Super League, na Kuta Collections, Mfalme FC pamoja na Chabaiywa FC zinazocheza katika ligi za chini.

Ushindi wa BB Bread dhidi ya Gor unatimiza ahadi yao, waliotoa baada ya kuwabandua AFC Leopards kwamba wembe uliokata kucha za chui, ungewanyoa Green Commandos.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

BB BREAD YABOMOA GOR, AFC LEOPARDS

RUTO: TUTAONGEA NA ODM KWA USAWA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *