STARS WAJIANDAA KUNG’AA KWENYE MASHINDANO YA FIFA
Timu ya taifa ya wanaume ya soka Harambee Stars inatarajiwa kuondoka leo nchini kuelekea Rwanda baada ya kufanya mazoezi yao ya mwisho hapo jana ugani Nyayo jijini Nairobi.
Stars watashiriki mechi za kirafiki katika mashindano ya 2026 FIFA Series, ambayo yamezinduliwa kwa lengo ya kuyawezesha mataifa fursa za kushiriki mechi za kimataifa.
Kocha mkuu Benni McCarthy, ameonyesha matumaini ya kikosi chake kufanya vyema licha ya kichapo cha mabao 8-0 na Senegal kwenye mechi yao ya mwisho ya kirafiki.
Mashindano hayo yatakayoanza hii leo na kuendelea kwa wiki moja, yatatumika kama maandalizi ya kipute cha mataifa bingwa barani Afrika, AFCON 2027, ambayo Kenya itakuwa mwenyeji.
McCarthy ametaja kikosi cha wacezaji 23, kinachowajumuisha wachezaji wakongwe na chipukizi ili kuimarisha ushindani.
Harambee Stars watachuana na Estonia Ijumaa wiki hii, kabla ya kupambana na Rwanda ama Grenada Jumatatu wiki ijayo, mechi zote zikiratibiwa kusakatwa katika uwanja wa Amahoro.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































