VIONGOZI WA PWANI WATAKA JOHO KUWA NAIBU RAIS 2027
Baadhi ya wanachama wa chama cha ODM kutoka eneo la Pwani wanaendeleza kampeni za kumtaka Waziri wa Madini, Hassan Joho, kuwa Naibu Rais mwaka 2027.
Wakiongozwa na Naibu Kiongozi wa chama na Gavana wa Mombasa, Abdulswamad Nassir, pamoja na Gavana wa Kilifi Gideon Mung’aro,viongozi hao wameonyesha imani kuwa chama kitashinda nafasi zote za uongozi.
Nassir amesema kuwa chini ya makubaliano ya serikali jumuishi, ODM itadai nafasi ya Naibu Rais, akimtaja Joho kuwa mgombea anayefaa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































