#Local News

WANGA AKANA LINDA MWANANCHI

Wakati uo huo, mwenyekiti wa kitaifa wa ODM Gladys Wanga, amepinga madai kwamba chama hicho kimegawanyika kwenye makundi mawili, akisema vuguvugu la Linda Mwananchi linaloongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna halina uhusiano na ODM.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha redio, Wanga amesema ODM iko imara, na kwamba matayarisho ya kongamano la kitaifa la wajumbe litakalofanyika hapo kesho yamekamilika.

Kulingana naye, ni unafiki kwa viongozi wa Linda Mwananchi kupinga uongozi wa kinara Oburu Oginga.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *