#Local News

MIGAWANYIKO ODM MKAKATI WA ODINGA, WAKILI ADAI

Imeibuka kwamba mrengo wa waasi wa Linda Mwananchi ndani ya chama cha ODM ukiongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna, ulipangwa kimaksudi na aliyekuwa waziri mkuu marehemu Raila Odinga kama mkakati wake mpana wa kuondoka kwenye ushirikiano wa kisiasa na Rais William Ruto endapo matakwa yake hayangetekelezwa.

Kwenye mahojiano, wakili Paul Mwangi, aliyekuwa mwandani wa siku nyingi wa Odinga, amesema kuwa kuwa mirengo miwili iliyo ndani ya ODM imekuwepo kwa muda mrefu, mmoja ukiwajumuisha viongozi wa kidiplomasia, na mwingine wa waasi.

Amesisitiza kuwa mirengo yote inawakilisha misimamo tofauti ya Odinga, aliyemtaja kama kiongozi mwenye nyuso nyingi za kisiasa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *