DCI YAFICHUA UOZO KATIKA KABURI LA PAMOJA KERICHO
Miili yote 33 iliyofukuliwa kutoka kaburi la pamoja katika eneo la Makaburini kaunti ya Kericho, ilitolewa katika makafani ya hospitali ya rufaa na mafunzo ya kaunti ya Nyamira, tofauti za taarifa za awali kwamba makafani hiyo iliruhusu miili 13 pekee.
Kulingana na mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa jinai, DCI, Mohammed Amin, uchunguzi wa awali na tathmini ya kamera za CCTV zimethibitisha kuwa miili yote ilitoka kwenye makafani hiyo.
Miongoni mwa wanaosakwa ni wazazi wa watoto 25 ambayo miili yao ilikuwa kwenye kaburi hilo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































