FAMILIA ZA WAATHIRIWA VITA URUSI ZALIA
Imeibuka kwamba familia za wakenya waliouawa kwenye mapigano kati ya Urusi na Ukraine wamepewa chaguo kukubali jamaa zao wazikwe nchini Urusi au miili yao ichomwe kisha watumiwe majivu.
Kulingana na familia hizo, idara inayosimamia wakenya walioko ughaibuni imezitaka kukubali jamaa zao wazikwe kwa heshima zote za kijeshi, au kuteketeza miili na kufanikisha usafirishaji wa majivu, familia hizo zikiilaumu serikali kwa madai ya kushindwa kuzisaidia licha ya ziara ya mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi nchini Urusi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































