#Business

IDADI YA WATALII YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 9 MWAKA 2025

Sekta ya utalii nchini Kenya imerekodi ukuaji imara mwaka 2025, huku idadi ya watalii wa kigeni ikiongezeka kwa asilimia 9. Ripoti iliyotolewa na Wizara ya Utalii na Wanyamapori ya nchini  imesema, sekta hiyo, ikichochewa na sera ya kufutwa kwa visa na kuongezeka kwa safari za ndege, imerekodi ukuaji endelevu mwaka 2025, na kuthibitisha tena nafasi yake ya kimkakati kama msingi muhimu wa uchumi wa taifa.

Vile vile ripoti hiyo imeonyesha kuwa, sekta ya utalii imeingiza shilingi nusu trilioni kwa mapato ya jumla, na kuakisi ufufukaji endelevu, uvumbuzi na maboresho ya utendaji.

Wizara hiyo aidha imesema, ukuaji huo pia unaakisi nafasi ya kimkakati ya Kenya ndani ya ulingo wa utalii duniani, hususan kutokana na ushindani wa vivutio vya utalii kwa ajili ya nafasi ya kupanua soko la kimataifa la usafiri.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

IDADI YA WATALII YAONGEZEKA KWA ASILIMIA 9 MWAKA 2025

KMPDU YADUMISHA UONGOZI WAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *