RUTO AONYA MAFISADI WA MAFUTA
Rais William Ruto ameonya kuwa wahusika wa mtandao wa ulanguzi katika sekta ya mafuta na petroli watakaotumia mgogoro wa Mashariki ya Kati kujinufaisha watakabiliwa na adhabu kali.
Rais amesema serikali haitaruhusu watu wachache kutumia hali ya mgogoro huo kuwanyanyasa Wakenya kupitia vitendo vya ufisadi katika sekta ya mafuta.
Akizungumza katika eneo bunge la Kilgoris, kaunti ya Narok, Ruto amesisitiza kuwa serikali yake itachukua hatua kali kuwaondoa walanguzi na makundi yote ya kifisadi katika sekta ya petroli.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































