#Basketball #Sports

NAIROBI CITY THUNDER WAMALIZA MASHINDANO YA AFRIKA KWA USHINDI

Derrick Ogechi alifunga pointi 22 na kuiongoza Nairobi City Thunder kumaliza mashindano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika kwa ushindi, baada ya kuwashinda RSSB Tigers ya Rwanda kwa mara ya kwanza katika michuano hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa SunBet Arena.

City Thunder, waliomaliza na ushindi wa michezo miwili na kupoteza mitatu, waliibuka na ushindi wa pointi 101-92 dhidi ya Tigers.

Kabla ya mchezo huo, Thunder tayari walikuwa wameondolewa katika mashindano, huku Tigers wakiwa tayari wamefuzu kwa hatua ya mtoano itakayofanyika Kigali mwezi Mei.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *