RUTO AMTETEA KINDIKI DHIDI YA UKOSOAJI
Rais William Ruto amemtetea naibu wake Kithure Kindiki dhidi ya wakosoaji, akimtaja kama kiongozi mnyeneyekevu huku akiwapuzilia mbali viongozi anaosema wanamdhalilisha Kindiki.
Rais alikuwa akizungumza katika kaunti ya Tharaka Nithi baada ya kuwakabidhi wafanyabiashara soko jipya mjini Chuka, akiipigia upato sekta za kilimo, afya na elimu.
Amewataka wakenya kuwapiga msasa viongozi kwa misingi ya utendakazi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































