#Football #Sports

MAN CITY, CHELSEA FAINALI ZA FA

Manchester City ilijikatia tiketi ya kushiriki fainali za dimba la FA, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia kwa klabu yoyote kucheza kwenye fainali za FA mara 4 mfululizo.

Mabao ya Jeremy Doku na Nico Gonzalez yaliiwezesha City kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 2-1 kwenye semi fainali dhidi ya Southampton ugani Wembley.

City watachuana na Chelsea kwenye fainali zitakazochezwa tarehe 16 mwezi ujao ugani humo, Chelsea wakisaka taji la kwanza la nyumbani tangu mwaka wa 2018.

Walifika fainali hizo kupitia bao la pekee la Enzo Fernandez dhidi ya Leeds United hapo jana.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MAN CITY, CHELSEA FAINALI ZA FA

BEI YA TANI YA MIWA YASHUKA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *