RUTO ATOA WITO WA MAGEUZI YA SEKTA YA AFYA AFRIKA
Rais William Ruto ametoa wito kwa mataifa ya Afrika kufanya mageuzi makubwa katika mifumo ya afya kwa kukumbatia ubunifu, ushirikiano na kujitegemea ili kuboresha huduma za afya
Akizungumza katika Mkutano wa Kikanda wa Afya Duniani jijini Nairobi Ruto amesema kuna pengo kubwa ambapo Afrika inabeba zaidi ya asilimia 25 ya mzigo wa magonjwa duniani lakini inapokea chini ya asilimia 3 ya matumizi ya afya kimataifa
Ameongeza kuwa bara linazalisha chini ya asilimia 2 ya dawa linazotumia hali inayodhihirisha utegemezi mkubwa wa uagizaji kutoka nje akihimiza uwekezaji zaidi katika uzalishaji wa dawa na kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































