#Local News

WAKILI ONGOYA AHOJI MISINGI YA KUMNG’ATUA GACHAGUA

Wakili Elisha Ongoya amesema tafsiri ya Mahakama ya Juu kuhusu “utovu mkubwa wa nidhamu” inahusisha makosa makubwa yanayoweza kuhalalisha kuondolewa madarakani.

Ongoya amesisitiza kuwa mashtaka ya aina hiyo yanapaswa kuwa mahususi na yenye uzito sawa na mashitaka ya jinai ili kukidhi viwango vya kikatiba vinavyohitajika katika mchakato wa kuondoa kiongozi madarakani.

Amehoji kuwa madai yaliyotolewa dhidi ya Rigathi Gachagua hayakufikia kiwango hicho na hivyo kuzua mjadala iwapo hatua hiyo ilikuwa ya kisiasa badala ya kisheria.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *