#Football #Sports

JOHN NJOGU AAGA KCB BAADA YA MKATABA KUISHA

Kocha mwenye uzoefu John Njogu ametangaza rasmi kuondoka katika klabu ya KCB FC baada ya mkataba wake kumalizika Aprili 26.

Kupitia mitandao ya kijamii, Njogu alitoa ujumbe wa hisia akitafakari safari yake ndani ya klabu hiyo, akishukuru kwa nafasi aliyopata na ushirikiano alioupata kutoka kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Njogu alijiunga na KCB mnamo Juni 2025 kama mkufunzi chini ya kocha mkuu Robert Matano ambapo alipata sifa kwa taaluma yake na uwezo wa kuchanganya mbinu za kisasa za mafunzo na mazingira ya soka la humu nchini.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *