#Local News

GACHAGUA ADAI MILIONI 80 KAMA FIDIA

Vikao vya kusikiliza kesi kuhusiana na mchakato wa kubanduliwa kutoka afisini kwa aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua vinaingia siku ya pili hii leo huku kiongozi huyo wa DCP akitaka mahakama iamuru serikali imlipe fidia ya shilingi milioni 80 na marupurupu ya kustaafu.

Wakati wa vikao vya siku ya kwanza, Gachagua ameiarifu mahakama kwamba hana haja ya kurejeshwa afisini ila anataka mshahara ya miezi 35 ambayo angehudumu iwapo hangebanduliwa kupitia mchakato anaosema ulikiuka katiba.

Miongoni mwa madai mengine ni malipo ya magari rasmi ya serikali ambayo angetumia kwa muda huo na pensheni ya laki tisa kila mwezi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

GACHAGUA ADAI MILIONI 80 KAMA FIDIA

MASOMO JSS NJIA PANDA MUHULA HUU

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *