MKENYA ATAKA KUFUTILIWA MBALI PENDEKEZO LA ADANI
Mkenya kwa jina Lango Guyo amewasilisha kesi katika mahakama ya Milimani akitaka kusitishwa kwa pendekezo la shirika la Adani Airport kupewa kandarasi ya kuukarabati uwanja wa ndege wa JKIA, akisema zoezi hilo lilifanywa bila kushirikisha wananchi na ukosefu wa uwazi, inavyohitajika kisheria.
Kwa mujibu wa Guyo, mchakato mzima wa utoaji wa kandarasi hiyo ulikumbwa na ukiukaji mkubwa wa sheria na kuitaka mahakama iizuie serikali dhidi ya kufanya ushirikiano zaidi na sekta ya kibinafsi kuhusiana na JKIA na raslimali nyingine muhimu ya taifa.
Hata hivyo, mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi amepinga taarifa kwamba serikali ina njama ya kuuza uwanja huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 
































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































