AJALI KAKAMEGA: FAMILIA YAOMBOLEZA JAMAA 2
Familia moja katika eneo la Sabatia kaunti ya Vihiga inaomboleza kifo cha jamaa zao wawili walioangamia kwenye ajali hapo jana jioni katika eneo la Iguhu, idadi ya watu waliofariki hadi sasa ikiwa 10.
Kwa mujibu wa familia hiyo, jamaa zao walikuwa safarini kutoka kwenye sherehe ya kifamilia katika eneo la Soy, wawili wakiangamia papo hapo huku wengine 4 wakiendelea kupokea matibabu.
Wameitaka serikali kuwasaidia kugharamia matibabu ya waathiriwa na mipango ya mazishi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































