MBADI ATETEA KUFURUSHWA KWA SIFUNA ODM

Muda mfupi baada ya seneta wa Nairobi Edwin Sifuna kutimuliwa kutoka wadhifa wa katibu mkuu wa chama cha ODM, Waziri wa fedha John Mbadi ametetea uamuzi huo, akisema Sifuna hakuwa chaguo bora kushikilia wadhifa huo. Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Mbadi amesema wadhifa huo ulistahili kupewa Wafula Buke kufuatia kuondoka kwa Ababu Namwamba, […]

HAVI ABATILISHA NIA YA JAJI MAHAKAMA YA UPEO

Aliyekuwa Rais wa chama cha wanasheria nchini LSK Nelson Havi, ametangaza kwamba hatawania wadhifa wa jaji wa mahakama ya upeo, ulioachwa wazi kufuatia kifo cha jaji Mohammed Ibrahim Disemba mwaka jana. Kwa mujibu wa wakili huyo mashuhuri, amechukua uamuzi huo baada ya mashauriano na wazee wa jamii ya Somali na Abaluhya, na kwamba amekubali kumuunga […]

SAKAJA: MAJUKUMU YA KAUNTI HAYAENDI SERIKALI KUU

Ushirikiano uliopo baina ya serikali ya kaunti ya Nairobi na serikali kuu hautasababisha uhamisho wa mamlaka na majukumu kwa serikali kuu bali unalenga kuboresha huduma kwa wakazi wa jiji la Nairobi. Haya ni kulingana na gavana Johnson Sakaja, akiwa mbele ya bunge la kaunti hiyo ambako amewaondolea wakazi hofu kwamba huenda baadhi ya majukumu na […]

KOCHA DE ZERBI AONDOKA MARSEILLE

Kocha Roberto De Zerbi ameondoka klabu ya Marseille kwa makubaliano ya pande zote, siku chache baada ya timu hiyo kuchapwa mabao 5-0 na mahasimu wao wakuu Paris Saint-Germain. Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 46, aliyekuwa akiongoza timu hiyo tangu kiangazi cha 2024, anaelezwa kuhusishwa na uwezekano wa kurejea Ligi Kuu ya Uingereza. Marseille ilitolewa […]

FAITH CHEROTICH KUFUNGUA MSIMU WA 2026 KWA MBIO ZA 5000M

Bingwa wa dunia wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi, Faith Cherotich, anatarajiwa kufungua msimu wake wa 2026 kwa kushiriki mbio za mita 5000 katika mkutano wa Riadha wa Athletics Kenya utakaofanyika Kapsabet mwezi Machi. Kocha wake, Bernard Rono, amesema Cherotich yuko katika hali nzuri ya mazoezi, huku programu yake ya maandalizi ikirekebishwa kidogo kufuatia […]

WAMBUA: NIDHAMU YA MBINU NI MUHIMU KWA SHUJAA

Kocha mkuu wa Kenya Sevens, Kevin Wambua, amesema usimamizi mzuri wa mchezo na nidhamu ya mbinu ndiyo yatakuwa mambo muhimu yatakayoamua hatima ya Shujaa katika mashindano ya World Sevens Division Two yanayoanza wikendi hii katika Uwanja wa Nyayo. Wambua amesema mashindano hayo ni makubwa zaidi kuwahi kuandaliwa nyumbani, huku fahari ya taifa na nafasi ya […]

OWINO AAMINI GOR MAHIA INAWEZA KUTWAA MATAJI MENGI

Beki wa Gor Mahia, Sylvester Owino, amesema K’Ogalo ina kila kinachohitajika kumaliza msimu kwa kutwaa mataji kadhaa, akisisitiza kuwa kikosi cha sasa kina uwezo wa kushindania ubingwa katika mashindano yote. Owino alizungumza siku chache baada ya Gor Mahia kuichapa Dero FC mabao 2-0 katika mechi ya raundi ya 64 bora ya FKF Cup iliyochezwa katika Uwanja wa […]

MWANAFUNZI WA GRADE 2 AGONGWA NA TREKTA KAKAMEGA

Hali ya huzuni imetanda katika eneo la Shilakwe, Navakholo, kaunti ya Kakamega, baada ya mwanafunzi wa darasa la pili kufariki dunia kufuatia kugongwa na trekta. Inadaiwa kuwa mwanafunzi huyo alikuwa akijaribu kuvuta miwa kutoka kwenye trekta lililokuwa likisafiri na kubeba mzigo wakati ajali hiyo ilipotokea. Wakazi wa eneo hilo sasa wanatoa wito kwa madereva kuwa […]

MURUNGI AKOSOA BARAZA LA MAGAVANA

Naibu Spika wa Seneti na Seneta wa Meru, Kathuri Murungi, amelikosoa vikali Baraza la Magavana kwa kutishia kususia vikao vya Kamati ya Ukaguzi wa Hesabu za Umma, akiwataka waboreshe utendaji wao au waachie nyadhifa zao. Murungi amekanusha madai ya magavana kwamba wanatishwa au kunyanyaswa wanapofika mbele ya kamati za Seneti, akisisitiza kuwa ukaguzi wa matumizi […]

OBURU AONYA VIONGOZI WA ODM KUHUSU NIDHAMU

Kiongozi wa chama cha ODM, Oburu Oginga, amewakosoa vikali maafisa wakuu wa chama wanaodaiwa kukiuka maamuzi ya vyombo muhimu vya chama, akionya kuwa ukosefu wa nidhamu miongoni mwa uongozi unatishia mshikamano wa ODM. Akihutubia kikao cha Kamati Kuu ya Kitaifa (NEC) kilichofanyika Mombasa, Oburu amesema baadhi ya wanachama wa Kamati ya Utendaji na Kamati Kuu wamekuwa […]