WAKENYA HALISI KUPOKEA VITAMBULISHO

Rais William Ruto amefafanua kwamba mageuzi ya serikali kuhusu utoaji wa vitambulisho vya kitaifa hayakufuta uthibitishaji wa uraia, akisisitiza kwamba ni raia halali wa Kenya pekee watakaopokea hati hizo. Akizungumza wakati wa sherehe za siku ya madaraka katika kaunti ya Wajir hii leo, Ruto amesema mageuzi yaliyoanzishwa na utawala wake yanalenga kukomesha ubaguzi dhidi ya jamii […]

SHEREHE ZA MADARAKA

Rais william ruto amewasili katika uwanja wa Wajir kwa ajili ya sherehe za siku ya madaraka ya 2026, ikiwa ni mara ya kwanza kwa hafla ya kitaifa kufanyika katika eneo la kaskazini mashariki mwa Kenya. Maadhimisho ya siku ya madaraka ya mwaka huu yatafanyika chini ya kaulimbiu, “elimu, ujuzi na mustakabali,”  huku serikali ikisema tukio hilo linalenga […]

LINDA MWANANCHI KUELEKEA THIKA

Mrengo wa Linda Mwananchi unatarajiwa kufanya mkutano wa mashauriano mjini Thika huku ukiongeza juhudi za kupanua ushawishi wake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Akizungumza katika mkutano wa kisiasa Kaunti ya Machakos Mbunge wa Suba Kusini Caroli Omondi amesema muungano huo una uwezo wa kujikusanyia hadi kura milioni 16 katika uchaguzi ujao. Mkutano wa Thika utakuwa wa […]

SERIKALI KUPANGA MAZISHI YA WANAFUNZI 16

Serikali imeunda kamati maalum ya kuratibu mazishi ya wanafunzi 16 waliofariki katika mkasa wa moto uliotokea katika shule ya Utumishi Girls Academy wiki iliyopita. Kwa mujibu wa afisa mmoja wa kamati hiyo, mwelekeo wa maandalizi hayo utatangazwa Jumanne, huku serikali ikiahidi kugharamia mazishi ya waliofariki pamoja na matibabu ya wanafunzi wanaoendelea kupokea huduma hospitalini. Hatua […]

UPINZANI WATAKA KATIBA IHESHIMIWE

Viongozi wa muungano wa upinzani wameitaka marekani kuheshimu Katiba ya Kenya pamoja na kutii amri za mahakama zilizositisha mpango wa kuanzisha kituo cha karantini ya Ebola nchini. Viongozi hao wamesema hatua yoyote inayohusu kuanzishwa kwa kituo hicho inapaswa kufuata sheria za nchi na kuhusisha wananchi kupitia mchakato wa ushirikishwaji wa umma. Aidha, wamependekeza kufanyika kwa kikao cha […]

TUZO YA BALLON D’OR KUFANYIKA LONDON

Sherehe za utoaji wa tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2026 zitafanyika kwa mara ya kwanza jijini London Oktoba 26 kuadhimisha miaka 70 tangu tuzo hiyo ilipotolewa kwa mara ya kwanza mwaka 1956. Waandalizi wamesema hafla hiyo itaadhimisha kumbukumbu ya mwanasoka wa Uingereza Stanley Matthews aliyekuwa mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni, tuzo […]

WAMOTO AIPA KABRAS NAFASI YA KUTWAA ENTERPRISE CUP

Kocha wa raga wa Chuo Kikuu cha Kibabii Peter Wamoto ameipa Kabras RFC nafasi kubwa ya kutwaa taji la Enterprise Cup katika fainali itakayochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa RFUEA Grounds. Kabras wanapania kutwaa ubingwa huo kwa mara ya sita mfululizo baada ya hivi karibuni kutwaa taji la Kenya Cup kwa mara ya tano mtawalia huku wakikabiliwa na […]

STARLETS YAJIANDAA KWA MECHI DHIDI YA UGANDA

Beki wa timu ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 Pauline Namisi pamoja na mshambuliaji Emily Adhiambo wamesema timu hiyo itategemea ukomavu, nidhamu ya kiufundi na sapoti ya mashabiki katika mechi ya marudiano dhidi ya Uganda. Wachezaji hao wameeleza kuwa sare ya mabao 1-1 waliyoipata katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika uwanja […]

MOTO WAZUKA SHULE YA GACHARAGE MURANG’A

Moto ulizuka usiku wa Alhamisi katika shule ya upili ya Gacharage eneo la Kandara Ruchu Kaunti ya Murang’a na kuzua hofu mpya kuhusu usalama wa taasisi za elimu nchini. Tukio hilo limejiri saa chache baada ya mkasa wa moto katika shule ya Utumishi Girls Academy eneo la Gilgil uliosababisha vifo vya wanafunzi 16 na kujeruhi wengine wengi […]

MAHAKAMA YASITISHA MPANGO WA KITUO CHA EBOLA

Mahakama Kuu imesitisha kwa muda mpango wa serikali wa kuanzisha au kuendesha kituo chochote cha karantini, kutenga au kutibu Ebola nchini Kenya chini ya makubaliano yoyote na Marekani au serikali nyingine za kigeni. Mahakama pia imezuia serikali kuwaruhusu kuingia nchini, kuwapokea au kuwahamisha watu waliothibitishwa au wanaoshukiwa kuathiriwa na virusi vya Ebola hadi kesi hiyo […]