WABUNGE, MASENETA KAZINI LEO

Maseneta na wabunge hatimaye wanarejelea vikao vyao hii leo bungeni baada ya likizo ya miezi 2, spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula akiratibiwa kukutana na viongozi wa bunge saa nne asubuhi kupanga namna vikao hivyo vitaendeshwa. Miongoni mwa masuala yanayotarajiwa kupewa kipaumbele kwenye mijadala ya bunge ni mpango wa serikali kuuza asilimia 15 za […]

MAGAVANA WADAI KUITISHWA HONGO NA MASENETA

Kamati ya seneti kuhusu uhasibu wa fedha za umma imepuzilia mbali madai ya kuwahangaisha na kuwaitisha hongo magavana wanaofika mbele ya kamati hiyo kutoa mwanga wa matumizi ya fedha za kaunti, ikisema magavana wanalenga kukwepa kutoa ufafanuzi kuhusu ubadhirifu wa fedha za umma. Mwenyekiti wa kamati hiyo Moses Kajwang’ ambaye pia ni seneta wa Homa […]

MAHANGAIKO YA WAGONJWA WA KANSA

Wagonjwa wa saratani nchini sasa wanalazimika kununua dawa nje ya hospitali licha ya kusajiliwa na bima ya afya SHA kutokana na uhaba wa dawa kwenye hospitali mbali mbali za umma. Baadhi ya wagonjwa hao katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta na AIC Kijabe, wamesema uhaba huo pia umeshuhudiwa kwa vifaa vingine vya matibabu. Sasa wameitaka […]

PSG KILELENI LIGUE 1

Ousmane Dembele alifunga mabao mawili huku Paris Saint‑Germain wakipiga Marseille kwa 5–0 Jumapili, wakirudisha kileleni mwa Ligi ya Ufaransa Ligue 1. Dembele alifungua bao dakika katika dakika ya 12 na kuongeza lingine kabla ya mapumziko huku PSG ikionesha nguvu kabla ya vipindi muhimu vya msimu. Bao la kujifunga la Facundo Medina na mabao ya nyongeza kutoka kwa Khvicha […]

WANG’AYA AJIUNGA NA NAIROBI UNITED

Kiungo wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Kevin Wang’aya, amejiunga na klabu ya Nairobi United akilenga kusaidia timu hiyo kufanya vyema na kupigania nafasi za juu msimu huu. Akizungumza wakati wa kutambulishwa kwake, Wang’aya amesema yuko tayari kwa changamoto mpya, akiahidi kuleta ubunifu, nguvu na udhibiti katika safu ya […]

WAITHIRA AONGOZA MBIO ZA UFUNGAJI KPL

Nahodha wa Murang’a Seal, Joe Waithira, ameonyesha nia thabiti ya kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu Kenya msimu wa 2025/26 baada ya kuongoza chati ya wafungaji kwa tofauti wazi. Waithira aliendeleza kiwango chake bora kwa kufunga mabao mawili na kuiongoza Murang’a Seal kuibuka na ushindi wa mabao 2–1 dhidi ya APS Bomet katika […]

JUMA : JUNIOR STARLETS WATAFUZU KOMBE LA DUNIA

Kocha wa Junior Starlets, Jackline Juma, amesema timu yake ina uwezo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake wasiozidi umri wa miaka 20 mwaka 2027. Kauli hiyo imejiri baada ya Kenya kuibuka na ushindi wa mabao 1–0 dhidi ya Tanzania katika mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa Uwanja wa Ulinzi Sports Complex. […]

BARASA NA SAVULA WADUMU SERIKALI JUMUISHI

Gavana wa Kakamega, Fernandes Barasa, amesema watasalia katika serikali jumuishi kwa kuzingatia msimamo na matakwa ya hayati Raila Odinga. Akizungumza katika kaunti ya Kakamega , kiongozi huyo amesema uamuzi huo unatokana na haja ya kudumisha umoja wa kitaifa na kuendeleza ajenda za maendeleo kwa manufaa ya wananchi. Aidha Barasa amesisitiza kuwa kushiriki kwao katika serikali jumuishi kunalenga kuhakikisha sauti ya wakazi wa […]

MARAGA AHIMIZA USAJILI WA WAPIGA KURA

Jaji Mkuu mstaafu David Maraga ameendeleza ajenda ya vuguvugu la UGM katika kaunti ya Garissa kwa kutoa wito wa kuimarishwa kwa usajili wa wapiga kura kote nchini. Akizungumza wakati wa mkutano na wakazi wa eneo hilo, Maraga amewataka hasa vijana kujitokeza kwa wingi kujisajili kama wapiga kura ili kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya uongozi wa […]

KALONZO ATETEA AZIMIO

Kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, ametetea muungano wa Azimio One Kenya akisema bado uko hai, siku chache baada ya kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi ndani ya muungano huo. Akizungumza katika jimbo la Maryland nchini Marekani, ambako, Kalonzo amezungumzia masuala ya kitaifa na umuhimu wa kudumisha misingi ya demokrasia. Aidha Kalonzo Amewahimiza Wakenya wanaoishi Marekani […]