MAHAKAMA YATOA AGIZO KWA POLISI KUHUSU BUNDUKI
Idara ya polisi imepewa makataa ya siku 90 kubuni mwongozo kuhusu matumizi ya bunduki miongoni mwa maafisa wake, ili kudhibiti visa ambapo baadhi ya maafisa hao wamekuwa wakitumia visivyo bunduki zao na kusababisha vifo vya raia.
Kwenye uamuzi wake alipoagiza fidia ya shilingi milioni 38.6 kwa waathiriwa 28 waliodhulumiwa na polisi wakati wa maandamano ya mwaka wa 2023 ya Okoa Uchumi jijini Kisumu, jaji wa mahakama kuu Alfred Mabea, amebaini ukiukaji wa wazi wa sheria kuhusu haki za kuishi na usalama wa wananchi.
Kati ya waathiriwa hao 28, 9 waliuawa wakati wa maandamano hayo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































