WIZARA YAONYA DHIDI YA DHULUMA ZA NGONO
Wizara ya elimu imeibua hofu kuhusu visa vya unyanyasaji wa kingono katika vyuo vya kiufundi, TVET, ikionya kuwachukulia hatua walimu wa taasisi hizo wanaojihusisha na visa hivyo.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Waziri wa elimu Julius Ogamba, amekiri kuwa wizara yake imepokea ripoti kuhusu unyanyasaji huo anaokariri kuwa unakiuka sheria za mafunzo nchini.
Kauli yake ikisisitizwa na katibu mkuu katika idara ya TVET Esther Mworia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































