SENETI YARATIBU KIKAO CHA HOJA YA MUTAI
Bunge la seneti limeratibu kikao maalum hapo kesho ambapo seneta maalum Consolata Nabwire aliyeteuliwa kujaza nafasi ya Gloria Orwoba ataapishwa, mbali na kujadiliwa kwa hoja ya kumbandua kutoka mamlakani gavana wa Kericho Eric Mutai.
Kwenye tangazo rasmi, spika wa seneti Amason Kingi amesema Nabwire ataapishwa saa nane unusu mchana, kabla ya maseneta kuangazia hoja ya kumbandua gavana Mutai.
Gavana huyo tayari alibanduliwa na bunge la kaunti ya Kericho, na hatma yake sasa imo mikononi mwa seneti ambayo imejipata chini ya madai ya kupokea hongo wakati wa vikao sawa na hicho.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































