HAKIMI NJE DHIDI YA BAYERN
Bingwa mtetezi wa dimba la klabu bingwa barani Ulaya, PSG, itakosa huduma za beki wake Achraf Hakimi katika mechi ya marudiano ya semi fainali ya dimba hilo dhidi ya Bayern kutokana na jeraha la paja.
Kupitia taarifa, PSG imesema raia huyo wa Morocco atakuwa nje kwa kile ilichotaja kama wiki chache kutokana na jeraha hilo.
Mabingwa hao watasafiri jijini Munich kuchuana na Bayern katika mechi ambayo wanaongoza kwa mabao 5-4 kutokana na ushindi kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.
Hakimi alionyesha maumivu katika dakika za mwisho kwenye mechi hiyo, akalazimika kucheza dakika zote ikizingatiwa kuwa tayari kocha mkuu Luis Enrique alikuwa amekamilisha mabadiliko yote.
Kutokana na pigo hilo, huenda Enrique akalazimika kumtumia kiungo Warren Zaire-Emery mwenye umri wa miaka 20 kama beki.
Mwingine ambaye pia atakosa mchuano huo ni kipa wa akiba Lucas Chevalier anayeuguza jeraha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































