#Football #Sports

KCB KUSAKA USHINDI MFULULIZO WA KWANZA MWAKA HUU

Timu ya KCB ina fursa ya kupata ushindi wa pili mfululizo kwa mara ya kwanza mwaka huu itakapochuana na Nairobi United ugani Ulinzi Complex leo alasiri.

Wenyeji Naibois wanaingia mechi ya leo baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Bandari FC, wakisalia katika nafasi ya 10 na pointi 29.

Wakati uo huo, wanabenki walionyesha mchezo wa hali ya juu walipoandikisha ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AFC Leopards wiki jana, ushindi uliowaweka katika nafasi ya 9 kwa pointi 32.

Hata hivyo, hawajapata ushindi mfululizo mwaka huu, na watalenga kufanya hivyo kwenye mechi ya leo, nao wenyeji wao wakilenga kufikisha mechi 3 bila kichapo.

Aidha, wanabenki hao watakuwa kwenye misheni ya kulipiza kisasi kufuatia kichapo cha mabao 2-0 na Naibois kwenye mechi ya mkondo wa kwanza Januari mwaka huu.

Ikiwa watashinda, KCB watachupa nafasi 2 hadi nafasi ya 7 juu ya Tusker FC na Bandari FC, na iwapo watapoteza, watashuka hadi nafasi ya 10 na kuwapa Naibois fursa ya kuingia nafasi ya 7 juu ya klabu hizo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KCB KUSAKA USHINDI MFULULIZO WA KWANZA MWAKA HUU

ROONEY ONYANGO APATA AFUENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *