FKF KUANDAA DROO YA FKF CUP
Shirikisho la soka nchini, FKF, linajiandaa kwa droo ya raundi ya 16 ya dimba la FKF Cup, baada ya raundi ya 32 kukamilika wikendi iliyopita.
Tayari miamba kadhaa wa soka nchini ikiwemo AFC Leopards na Gor Mahia zimebanduliwa baada ya raundi 2 pekee, na timu ya BB Bread inayoshiriki ligi ya FKF tawi la Nairobi East.
Leopards walibanduliwa katika raundi ya 64 huku Gor wakirambishwa sakafu katika raundi ya 32 na timu hiyo ya ligi ya chini.
Hata hivyo, timu 11 zinazoshiriki ligi kuu, KPL, wakiwemo mabingwa watetezi Nairobi United, zingali kwenye kinyang’anyiro hicho.
Jumla ya timu 16 zinasubiri kufahamu wapinzani wao kwenye raundi hiyo kabla ya robo fainali.
Bingwa wa FKF Cup atapata fursa ya kushiriki dimba la mashirikisho ya CAF msimu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































